Mahakama Yamkuta na Kesi ya Kujibu Mwijaku Katika Shtaka la Kusambaza Picha za Utupu

0

 Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, imemkuta na kesi ya kujibu msanii wa maigizo,Mwemba Burton maarufu kwa jina la Mwijaku, kwa kusambaza picha za utupu.

Uamuzi huo umetolewa Mei 5, 2022 na Hakimu Mkazi, Rhoda Ngimilanga, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wa mashahidi watano na vielelezo vinne.


Mwinjaku, ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach, anakabiliwa na shtaka la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria za nchi.

Anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019 katika jiji la Dar es salaam.

Katika kipindi hicho, Mwijaku anadaiwa kuchapisha picha za ngono kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp uliounganishwa katika kompyuta.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza picha hizo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Kwa uamuzi wa huo, Mwijaku atatakiwa kujitetea dhidi ya shtaka linalomkabili.

Mwijaku ameieleza mahakama kuwa atajitetea kwa kiapo na kwamba anatarajia kuita mashahidi watatu kupangua shitaka linalomkabili.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 10, 2022 ambapo Mwijaku ataanza kujitetea.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top