Jeshi la polisi mkoani kagera linamshikilia Maiko Martine miaka ( 30 )mkazi wa mtaa wa Kyabitembe Kata Nshambya Tarafa Rwamishenye Manispaa ya Bukoba kwa tuhuma za kubaka watoto watatu wa darasa la tatu na la nne wa shule ya msingi Ithawa wenye umri kati ya miaka (10 )na (12 ).

Kamanda Maketi Msangi, amewaeleza waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo February 23 ,mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika msitu wa serikali wa Rwendimi uliopo Kijiji cha Ijuganyundo Manispaa ya Bukoba.
SOMA HII;FAHAMU MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUKOSA HISIA ZA MAPENZI
Alisema siku hiyo watoto hao walikuwa wameenda kuokota kuni kwenye msitu huo ndipo mtuhumiwa aliwavizia akawakamata na kuwatishia kuwakata na panga kama watapiga kelele na kisha kuwabaka .
Alisema baada ya kufanya kitendo hicho cha kikatili mtuhumiwa alikimbia kusikojulikana na kuogopa kukamatwa .
Alisema watoto hao walimtambua mtuhumiwa aliyewabaka kwa sura na alikamatwa Mei 24,mwaka huu majira ya saa moja na dakika hamsini jioni Kijiji cha Kyansonzi Kata ya Maruku halmashauri ya Bukoba.
Katika tukio lingine kamanda amesema wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumuua Pankras Petro (62) mkazi wa Nyabishenge, wilayani Kyerwa, baada ya mdogo wa marehemu aitwaye Dominick Petro kuwakodisha watu watatu kwa ujira wa shilingi 50,000, ili wamuue kaka yake kutoka na mgogoro wa shamba.
SOMA HII;FAHAMU MAMBO YANAYO CHANGIA MWANAMKE KUKOSA HISIA ZA MAPENZI
"Walimjeruhi vibaya Pankras kwa kumkata na kitu cheye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, alikimbizwa hospitali ya Mission ya Isingiro na alifariki siku hiyo akipatiwa matibabu, watuhumiwa hao walikimbilia kusikojulikana, tulianza msako na kuwakamata Mei 25 baada ya kupata taarifa za siri," amesema Msangi.