MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA 6 ARUSHA

0

 WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji la Arusha akiwemo Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dkt. John Pima kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

Waziri wa Tanzania Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Jumanne, Mei 24, 2022, wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Jiji la Arusha na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwenye ukumbi wa AICC jijini humo.

Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mweka Hazina wa Jiji, Bi. Mariam Shaban Mshana; Bw. Innocent Maduhu (Mchumi), Bw. Alex Daniel Tlehama (Ofisi ya Mchumi, Bw. Nuru Gana Saqwar (Ofisi ya Mchumi) na Bw. Joel Selemani Mtango, Afisa Manunuzi  ambaye alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

SOMA HII: SABABU ZA WANAWAKE KUBRID DAMU NYINGI NA MUDA MREFU.

Amesema amefikia uamuzi huo kwa  kuwa hawezi kuvumilia kuona fedha za umma zikitumika kinyume na taratibu na akamuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa afuatilie masuala hayo hadi ijulikane ni akina nani waliohusika katika ubadhirifu huo.

“ Mdhibit na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG ingia kazini mara moja, tafuta nyaraka zote na wakati huo watumishi hawa watakaa pembeni kupisha uchunguzi hadi kazi hiyo itakapokamilika,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

SOMA HII: SABABU ZA WANAWAKE KUBRID DAMU NYINGI NA MUDA MREFU.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema timu nyingine za uchunguzi zilizokuwa zikifanya kazi kwenye suala hilo ziache mara moja na kuiacha timu maalumu ya uchunguzi ya CAG ifanye kazi yake Timu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top