MAJONZI;MWINGINE TENA AFIA MAJINI AKIOGELE KWENYE RAMBO

0

 Katamala Jackson mkazi wa kijiji cha Nyabange Wilayani Butiama Mkoani Mara amefatiki dunia wakati akiogelea katika lambo la maji akishindania shilingi elfu nne waliyowekeana na wenzake kwa ajili ya kushindana kuogelea katika bwawa hilo

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Kikosi cha zimamoto na ukoaji mkoani Mara  Agustino Magere amesema kikosi hicho kwa kushirikiana na wananchi waliweza kuopoa mwili wa kijana huyo ambae alikuwa tayari amefariki.

"Niwaase vijana kuacha kubeti kwa jambo ambalo linahatarisha maisha leo hii shilingi elfu nne imeweza kuondoa uhai wa mtu " alisema Magere.

Mwenyekiti wa Serikali ya kitongoji cha Manyala Kitende  Wambura amesema kijana huyo alikuwa akijishuhulisha na udereva wa pikipiki kijijini hapo huku ndugu wa marehenu huyo alisema wamempoteza ndugu yao ambae alikuwa tegemeo katika familia yao.

"Kumekuwepo na mazoea ya baadhi ya watu kuoga katika rambo hili la maji watu wazima na watoto lakini hili lambo limejengwa mahususi kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu na mifugo lakini kifo hiki kimetushitua" alisema Wambura Mwenyekiti wa kitongoji.

Aidha katika hatua nyingine kamanda Magere anapiga marufuku mtu yeyote kuogelea katika bwawa hilo na kuwataka viongozi wa serikali katika kitongoji hicho  kuyasimamia maagizo yake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top