Matukio 275 ya ukatili yameripotiwa mkoani Njombe

0

Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya familia ulimwenguni,takribani matukio 275 ya ukatili mkoani Njombe yameripotiwa katika dawati la jinsia na kufayiwa kazi katika kipindi cha kuanzia january hadi machi 2022 mwaka huu. 

Katika mkutano wake na waandishi wa habari,mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba amesema hali ya mikasa ya ukatili ndani ya familia yanazidi kukua na kudai kwamba kwa kiasi kikubwa chanzo kilichobainika kusababisha matukio hayo ni pamoja uwepo wa mila potofu na kandamizi na tamaa ya kupata utajiri.

“Kwa mujibu wa taarifa ya makosa ya ukatili na unyanyasaji kupitia jeshi letu la polisi kwa kipindi cha januari hadi machi 2022 jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia yaliyoripotiwa ni 127,yaliyoripotiwa na kushughulikiwa na afisa ustawi wa jamii katika ngazi ya halmashauri ni 275.”alisema Kindamba

Vile vile Kindamba ametoa wito kwa jamii mkoani humo kuongeza upendo katika familia zao ili kuleta amani na kukuza vipato vya familia na Taifa kwa ujumla.

Aidha Kindamba amempongeza Rais Samia kwa kuongeza kiwango cha mshahara kwa watumishi.

“Jana Mh Samia Suluhu Hassan ameongeza mshahara kima cha chini kwa 23.3% tunaamini kupanda kupanda huku kunaenda kuleta utulivu katika familia zetu tunamshukuru sana Mh Rais kwa kuwa na huruma na Watumishi wa serikali”Aliongeza Waziri Kindamba

Elice Simonile ni afisa maendeleo mkoa wa Njombe anasema mikasa ya ukatili hususani kwa watoto na akina mama inazidi kuongezeka kwasababu ya kuongezeka kwa usiri katika familia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top