Mbaroni tuhuma kumfanyia ukatili wa kingono mjukuu

0

Jeshi la Polisi mkoani Iringa, linamshikilia Desderia Mbwelwa (56), mkulima wa Lumuli Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kumfanyia ukatili wa kingono mtoto wa miaka minane.

 Mtoto huyo mwanafunzi wa darasa la tatu alikamatwa na mwanamke huyo na kuvutwa vichakani kisha kumlazimisha afanye tendo la ngono.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kitendo hicho kilimsababishia mtoto huyo maumivu makali sehemu za siri.

SOMA HII! Fahamu madhara PID na namna ya kujikinga nao

Alisema tukio hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu, majira ya saa 10 jioni, na tayari mtuhumiwa huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Wakati huo huo, watu watatu walikamatwa katika nyumba za kulala wageni mjini Iringa kwa tuhuma za utapeli, akiwamo Joseph January (28) maarufu kama Mgawe, aliyejifanya mganga wa kienyeji wa kusafisha nyota ya bahati kwa kumwingizia dawa mwanamke kwa kutumia sehemu zake za siri.

Kamanda Bukumbi alisema watuhumiwa hao walikamatwa Mei 12, mwaka huu, majira ya saa tatu usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Wihanzi na Udzungwa mjini Iringa.

Wengine walikamatwa kwenye nyumba za wageni eneo la Kihesa na Makorongoni, huku akiwataja kuwa ni January ambaye ni mkulima mkazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam, Richard Joseph (24) mkulima wa Sumbawanga na Revold Baruti (23), mkazi wa Sumbawanga.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na mabunda ya karatasi nyeusi zilizokatwa na kupangwa mfano wa noti za Tanzania na uchunguzi wa awali ulibaini walipanga kufanya utapeli huku wakitumia gari aina ya Mark X yenye namba za usajili T 979 DWN inayomilikiwa na Herieth Khamis, mkazi wa Dar es Salaam.

SOMA HII! Fahamu madhara PID na namna ya kujikinga nao

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top