Amesema “Hii sheria ya elimu ya mwaka 1978 ifanyiwe marekebisho, hii itaondoa mwanya wa Mawaziri wa nchi hii kuamua wanavyotaka kwenye elimu yetu.
"Kuna maamuzi ya ovyo yamewahi fanyika nchi hii, kuna waziri amewahi kuamka na kufuta UMITASHUMTA, kuna waziri amewahi kuchanganya Chemistry na Physics kuwa somo moja, kuna waziri amewahi kuondoa Division na kuleta GPA kwenye ufaulu kidato cha nne, haikubaliki kabisaaa.
“Nelson Mandela kwenye kitabu chake cha ‘The Long Walk to Freedom’ anasema "Education is the strongest weapon you can use to change the world", sisi kama taifa lazima tulinde mfumo wetu wa elimu usiingiliwe na Mtu mmoja au kikundi flani, lazima kuwe na ‘Public Opinion’ kwenye mabadiliko yoyote yanatakiwa kufanyika..
Aidha amesema kushuka kwa ubora wa elimu kwenye vyuo inasababishwa na vyuo kuondoka kwenye msingi wake wa awali wa kunzishwa.
“Uanzishwaji wa vyuo mbalimbali nchini ulikuwa na malengo mahususi kwa kila chuo, mfano SUA hiki kilikuwa maalumu kwa ajili ya Kilimo lakini leo wanatoa kozi za education (elimu).
“Mzumbe ni chuo maalumu cha Sheria,Uongozi na Utawala lakini leo wanatoa Education na Tourism (elimu na utalii)
Ardhi Chuo cha Maalum kwa ajili ya maswala ya Ardhi lakini leo kinatoa Accounts & Finance.
Mnataka hadi IFM nacho kianze kutoa Education? " anahoji Sanga.
"Lazima kama Taifa turudishe misingi ya kuanzishwa hivi vyuo, DUCE kama ilianzishwa kwaajili ya Ualimu ifanye ualimu na kama wanafunzi wanakuwa wengi wafungue Branch za DUCE mahali pengine na sio kuchanganya mambo eneo moja.
"Mh waziri wewe ni msomi tunakuomba sanaa sanaaa ufanye marekebisho kwenye vitu hivi, vyuo vinaongeza Idadi ya kozi ili kupata fedha nyingi za kujiendeshea. Haikubaliki kabisa".
“Utitiri wa vitabu kwenye mfumo wetu wa elimu ambavyo vingi havina ithibati na havina ubora wowote, tunaua elimu yetu kwa makusudi.” amesema