MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe, amekemea vikali tabia ya baadhi ya vijana wa chama hicho kuwavunjia watu heshima kwenye mitandao ya kijamii, hususani wale wanaotofautiana mitazamo.
Mbowe ameyasema hayo akihutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema unaoendelea kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amewakemea vijana wenye tabia hizo na kuwataka wawe na heshima na staha hata kwa watu wanaotofautiana nao kifikra.
“Tumewaita wanachama wetu 19, nashukuru wameheshimu wito, wamekuja kusikiliza rufaa yao, naomba niwatangazie kuwa wote wamefika na wapo kwenye vyumba hapa Mlimani City,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa:
Imesomwa zaidi:MBUNGE ATAKA SOKWE WAONDOLEWE KWENYE HISTORIA YA BINADAMU
“Nafasi ya chama chetu leo ni chama kikuu cha upinzani nchini, haina maana nafasi hiyo tukawa nayo siku zote, inawezekana kesho chama kikuu cha upinzani kikawa CUF, NCCR Mageuzi, ACT Wazalendo au vinginevyo, hivyo isiwe sababu ya kudhalilisha vyama vingine, hili ni lazima liachwe.
“Nilivyopata mwaliko kwenda Ikulu sikujitia kiburi kukataa. Wajibu wangu kama kiongozi ni kuweka vitu vingine chini, ili kusimamia maslahi na masuala ya kuinua Taifa hivyo nilikwenda Ikulu.”