Mbunge wa Manonga, Seif Gulamali ametaka mtaala wa somo la historia ufutwe akidai kuwa unawadanganya wanafunzi.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2022/2023 bungeni Jumatano Mei 11, 2022. Picha na Merciful Munuo |
Gulamali amesema habari ya kuwaambia wanafunzi kwamba binadamu alitokana na sokwe siyo kweli kwa sababu hadi sasa wapo Sokwe lakini hawajawahi kugeuka kuwa binadamu.
"Wanadamu wote tunazaliwa, tunazeeka na tunakufa na sokwe wanazaliwa wanazeeka hadi kufa bila kugeuka kuwa binadamu kwa nini tudanganye watoto," amesema Gulamali.
SOMA HII:HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WALIVYOWASILI MLIMANI CITY
Mbunge huyo amesema kama somo hilo litaendelea, kuna wakati mitaala itasema mbwa anaweza kugeuka kuwa simba au mbuzi atakuwa na kuwa ng'ombe.
Amesema elimu za namna hiyo ndiyo maana watoto wengi hawasomi historia kwani makanisani wanafundishwa vingine na wakienda shule wanafundishwa mambo mengine tofauti.
Kingine mbunge huyo ametaka idadi ya masomo kwa wanafunzi wa madarasa ya chini ipunguzwe ikibidi yawe manne au matano tu.