MDEE NA WENZAKE KUSALIA BUNGENI HADI JUNI 13

0

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesema wabunge 19 wa Chadema akiwemo Mdee na wenzake waliovuliwa uanachama wa chama hicho hivi karibuni wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania hadi Juni 13, 2022 Mahakama itakaposikiliza maombi yao ya zuio la muda.

Uamuzi huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jaji wa Mahakama Kuu, John Mgeta wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa, ambapo maombi yao namba 13/2022 ni maombi madogo kwenye shauri la msingi namba 16/2022, wabunge hao wanaiomba mahakama kurejeshewa uanachama wao .

Uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa wabunge hao umefanywa na Baraza Kuu la Chadema Mei 12, 2022 jijini Dar es Saaam katika ukumbi wa Mlimani City ambapo maombi hayo ya Mdee na wenzake yamefunguliwa dhidi ya bodi ya wadhamini ya Chadema, Tume ya Taifa ya uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mdee na wenzake wamefungua maombi ya zuio la muda wakiomba waendelee kuwa wabunge hadi uamuzi wa maombi yao utakapotolewa mahakamni hapo.

Awali ndani ya mahakama, Wakili Peter Kibatala, Jeremiah Mtobyesya ambao ni mawakili walioiwakilisha Chadema mahakamani hapo, walowasilisha hoja sita za kupinga kukubaliwa kwa zuio hilo, ambazo zilizojikita kwenye madai ya kasoro zilizopo kwenye hati ya kiapo cha waombaji.

Kibatala amedai Mahakamani hapo kiapo kina dosari ya kutotanabaishwa dini za waapaji (Mdee na wenzake), "Viapo vyao mavitaji dini zao ikitokea wanataka kuupa wataapa kwa kitabu gani?".

Ameeleza kuwa Hoja nyingine Kibatala amedai Mahakamani hapo waombaji wameomba waendelee na nyadhifa zao bila kueleza hoja hiyo inakwenda kwa nani, kama ameelekezwa Spika wa Bunge au Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Wakili wa Chadema John Malya, amewaeleza waandishi wa habari kuwa wamekubaliana kwa pamoja kusikiliza mashauri hayo ifikapo June 13 mwaka huu, ambapo upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bodi ya wadhamini wa Chadema watawasilisha hoja zao
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top