MFANYABIASHA HAUTAKIWI KUKOSA APLIKESHENI HIZI KWENYE SIMU YAKO.

0

- Apps Za Mitandao Ya Kijamii(Whatsapp Business, Facebook, Instagram, Twitter, Telegram Na Tiktok); Ukishakuwa Nazo Hakikisha Unaziweka Sehemu Mmoja Kwenye Bio Yako Ili Mteja Wako Aweze Kukufollow Sehemu Zote.

- App Ya CANVA; hii itakusaidia kudesign na kutengeneza posts zako za kila siku za kupost kwenye Akaunti zako mitandaoni. Ukiweza kutumia app ya CANVA utapunguza gharama nyingi sana za kulipa graphics designer mara kwa mara kukutengenezea matangazo ya posts, utatengeneza mwenyewe posts za kuvutia sana kwa ajili ya kuposti kwenye akaunti zako mitandaoni.


- App Ya KUZA BUSINESS; Hii itakusaidia kutunza taarifa zako za biashara Kama mauzo pamoja na mipango yako ya biashara.


- App Ya BUFFER; Hii itakusaidia kuposti kipindi ambacho upo bize au hauna bando.Kupitia App ya BUFFER Unaweza kuandaa posts za kuposti wiki nzima au mwezi mzima ukaweka na muda kisha muda huo ukifika posts hizo zitajiposti kwenye akaunti yako hata kama wewe upo bize, hii inasaidia unakua active muda wote kwenye kuposti.


- App Ya VPN ; kuna kipindi internet inakua inasumbua kwasababu za kimazingira, mfano mwaka jana ilikua hauwezi kutumia TWITTER Tanzania mpaka utumie VPN hivyo kama ungekua unatumia TWITTER kufanya biashara na hauna VPN bila shaka biashara yako ingeathirika.


- App Ya @SWAHILIESPAY kama unawateja nje ya nchi basi hakikisha unadownload na unawasiliana na @swahiliesapp ili uweze kutumia app yao kupokea malipo ya wateja wako wa nje.


- MPESA APP Na AIRTEL MONEY APP; kama hauna akaunti ya benki bila shaka utashindwa kufanya Matangazo ya Sponsored Ad kwani hautakuwa na njia ya kufanya malipo, lakini kama hauna akaunti ya Benki lakini una App Ya AIRTEL MONEY AU MPESA Ni rahisi kutengeza kadi ya benki(Virtual mastercard) kupitia Mpesa yako au Airtel Money Yako Na Kisha kufanya malipo ya Sponsored Ad bila kuwa na akaunti ya Benki.


- App Ya ENPASS; itakusaidia kutunza password zako za akaunti zako zote sehemu moja.

Credit; Kuza business

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top