MGANGA MBARONI KWA KUMTAPELI MBUNGE!

0

 Mganga mmoja raia wa Mali anayetuhumiwa kumlaghai mbunge wa zamani Danson Mungatana KSh 76 milioni ameambia mahakama kuwa alisusia vikao kwa sababu alikuwa mgonjwa.

Abdoulaye Kouro anayedaiwa kumlaghai Mungatana KSh 76 milioni kwa kisingizio kwamba angemwekeza katika sekta ya mafuta, alisema amekuwa akijitibu akitumia dawa za kienyeji.

              

 Kouro alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani ambapo alimuomba kuondoa hati ya kukamatwa kwake iliyotolewa akidai kuwa ni mgonjwa. 

"Mheshimiwa, nimekuwa mgonjwa, Sikwenda hospitali yoyote, nilichagua kujitibu kwa dawa za mitishamba” alisema Abdoulaye. 

Kuoro ambaye yuko rumande baada ya mahakama kufuta masharti ya dhamana, aliiomba korti imsamehe kwa kushindwa kupata stakabathi za matibabu za kuthibitisha kuwa amemponya.

 Anadaiwa kufanya kosa hilo kati ya Aprili 20 na 29,2013, katika ghorofa ya Sandalwood, kando ya barabara ya Brookside huko Westlands, kaunti ya Nairobi, pamoja na wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama.

 Kulingana na stakabathi za mashtaka, mganga huyo anadaiwa kuchukuwa kiasi cha dola 1,000,000 kutoka kwa Danson Mungatana, ambazo ni KSh 76,000,000 akijifanya kuwa ana uwezo wa kuwekeza kwa niaba yake katika biashara ya mafuta. 

Kouro pia alishtakiwa kwa kuwa na karatasi zilizokusudiwa kufanana na kupitisha kama noti za sarafu akijua kuwa ni za kughushi, Hakimu Mkuu Wendy Micheni alimweka rumande mganga huyo akisubiri kusikilizwa kwa kesi hiyo. 

Polisi wamewapanga Mungatana na Muteke kama mashahidi. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top