MHANDISI WA MRADI AKUTWA AMEKUFA HOTELINI TANGA

0

 

Raia wa Afrika kusini ambaye ni mhandisi mshauri katika mradi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Nchini Uganda-Tanga upande wa Tanga amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli aliyokuwa amepanga kwa muda wa mwezi mmoja na nusu.


Raia wa Afrika Kusini aliyetambulika kwa jina la Abraham Jacobus amefariki Dunia katika chumba cha Hoteli ya (Tanga beach) jijini Tanga alipokuwa amepanga

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga David Chidingi ni kuwa mtaalamu hiyo alifariki usiku wa kuamkia leo jumapili.

Mwili umehifadhiwa katika hopsitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Imeelezwa kuwa Abrahamu ana takribani mwezi mmoja na nusu akiishi katika hoteli hiyo na kwamba umauti umempata usiku wa kuamkia leo akiwa peke yake chumbani kwake.

Raia huyo wa Afrika kusini mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi katika mradi wa bomba la mafuta kwa upande wa Tanga kama Mhandisi Mshauri.

" Dereva wake wakati alipomfuata kwa lengo la kumchukua kuelekea kazini alimpigia simu kwa muda mrefu haikupokelewa na ndio akatoa taarifa kwa uongozi wa hoteli na wakafungua na kumkuta amefariki na wakatoa taarifa polisi " amebainisha Kaimu Kamanda Chidingi.

Amesema uchunguzi wa awali umebaini alikuwa na tatizo la athma na kwamba mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa uchunguzi zaidi.

"Marehemu ni raia wakigeni hivyo kuna taratibu ili kufanya uchunguzi wa kina na kubaini hasa chanzo cha kifo chake", amesema Kaimu kamanda huyo.

Chanzo - EATV 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top