Mwanamke mmoja nchini Serbia kwa jina la Teresa Peric (46) akidaiwa kumuua mumewe aliyefahamika kwa jina la Srdjan Peric (42). Tukio ambalo limetokea Mei 10, 2022 majira ya saa 3 za usiku.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, Teresa alimuwekea madawa kwanza ndipo akaanza kumchomachoma mumewe huyo kwa kisu na kumkatakata kisha kuyapika mapande ya mwili wa mumewe katika oven hob zikiwemo hizo korodani alizozikata kwa msumeno (chainsaw).
Binti wa mwananke huyo amedaiwa kushuhudia kila kitu na alienda kumuita kaka yake lakini na wao walianza kutishiwa na mama yao.
Kwa mujibu wa taarifa, Teresa na Peric walianza kuishi pamoja miaka miwili iliyopita na hawajazaa pamoja mtoto lakini kila mara wamekuwa wakishushiana vipigo na pia wote wanadaiwa kutumia madawa na wote wanaelezwa kuwa na matatizo ya akili ingawa haijathibitishwa na madaktari.
Teresa alishaolewa mara nne na kila ndoa amezaa mtoto mmoja hivyo ana watoto 4 kila mmoja na baba yake, lakini aliyemuua hawajazaa hata mtoto pamoja.
Siku moja hivi karibuni Teresa alidaiwa kupeleka moto kitandani alipokuwa amelala mumewe huyo kwa lengo la kumuunguza.
Mara kwa Mara waligombana huku mke huyo akimtuhumu mumewe huyo kuwa mvivu.