MKE NA MUME MBARONI KWA KUIBA NYANYA BUSTANINI.

0

Wakazi wawili wa Halmashauri ya mji wa Geita ambao ni Mtu na mkewe wamekamatwa na Wananchi wa Mtaa wa Lwenge kwa madai ya kuiba nyanya Kwenye bustani.

Mashuhuda wamedai kuwa Khamis Hassan ana tabia ya kuingia katika bustani za watu na kuiba miwa na leo aliingia kwenye shamba la Marselina Damaseni na kuanza kuvuna Nyanya.

Baadhi ya Wananchi waliokua karibu na kushuhudia Khamis akivuna nyanya walimfuata na kumhoji naye akadai anakwangua miwa ya Mzee Lema kwani ameagizwa kufanya hivyo.

Hata hivyo Khamis aliingia mtegoni kwani hazikuzaa matunda kwani aliambatana na Mkewe Ester Edward ambae naye alipewa jukumu la  kubebe Nyanya hizo anazoiba mumewe na hivyo wote wawili kuingia mbaroni kwa tuhuma za wizi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top