MKURUGENZI MAKETE ATOA SABABU KWANINI AMEWATAKA WANANCHI KUZALIANA ZAIDI.

0

 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe amesema wilaya ya Makete inahitaji kuongeza idadi ya watu kwa kuzaliana hivyo ameishauri wenye uwezo wa kuzaa kuendelea kuzaa.

 "Makete tusiwe na uzazi wa Mpango" Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete William Makufwe


Akizungumza na wananchi kwenye Mikutano mbalimbali ya kusikiliza na kutatua changamoto Kijiji kwa Kijiji, akiwa Kata ya Ukwama na Ipepo amewaomba wananchi hao kuzaliana kwa wingi ili kuongeza idadi ya wananchi Makete Mkoani Njombe.

@makufwe amesema "nafikiri Makete tusiwe na uzazi wa mpango bali tuzaliane kwa wingi na tufanye kazi kwa bidii ili kukuza pato la Uchumi kuanzia kaya, Kijiji, Wilaya na nchi kwa ujumla kwa kuwa tukiwa na fedha ndipo tutaweza kulea familia zetu vizuri".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top