MORRISON ASHIKILIWA NA POLISI KWA MADAI YA KUJERUHI

0

Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison anashikiliwa katika kituo Cha Polisi Cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumjeruhi shabiki wa Yanga na kitu chenye ncha kali. 

Akizungumza Mkuu wa Kituo Cha Polisi Chang’ombe, ASP Mohammed Simba ambapo amethibitisha kupokea kesi hiyo

 “Ndio tumepokea hiyo kesi na tunaendelea na mahojiano tukikamilisha tutawajulisha,” 

Tukio hilo limetoka mara baada ya Derby ya Kariakoo kutamatika katika uwanja wa Benjamin Mkapa April 30 2022. 

Mchezaji wa Simba Bernard Morrison anashikiliwa Kituo cha Polisi cha Chang'ombe ,kwa kosa la kuwachoma na kitu chenye ncha kali Mashabiki wawili wa Yanga na kumpiga Shabiki mmoja wa Simba waliokuwa wanamzomea. 

Morrison hakupanda Basi la timu baada ya mechi kumalizika ,na badala yake alipanda Gari yake ndogo kabla ya tukio kutokea. 

Inadaiwa kabla ya kupanda kwenye Gari Mashabiki walianza kumzomea , hivyo aliamua kuingia mbele kwenye Gari ambapo alitoka na kitu kinachodaiwa kuwa ni bisibisi na kuwakimbiza Mashabiki hao kisha kufanya vitendo hivyo. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top