MUME AKODI WATU WAKUMBAKA MKEWE KISHA KUMUUA

0

Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara linawashikilia watu wawili na kumtafuta mwingine mmoja kwa tuhuma za kumbaka kisha KUMUUA Elizabeth Steven Peter (41) Mkazi wa kijiji cha Mkajamila, wilaya ya Masasi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara ACP Nicodemus Katembo kwamba mnamo tarehe 06.05.2022 katika kituo cha Polisi wilaya ya Masasi kuliripotiwa tukio la kukutwa mwili wa Mwanamke mmoja aitwaye Elizabeth Steven Peter maeneo ya Mkunguni kata ya Migongo.

Inaelezwa kuwa baada ya uchunguzi wa mwili kufanyika ilibainika kuwa marehemu alibakwa kisha kuuawa kwa Kuvunjwa mifupa na shingo.

SOMA HII;Wasiojulikana wachoma gari la hakimu

Jeshi la Polisi lilianza kufanya upelelezi kuhusiana na tukio hilo ambapo kupitia wataalam wa cyber alikamatwa Innocent John Ndomba,(,32) Mkulima Mkazi wa Nangaya, katika mahojiano mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio kwa kukushirikiana na mume wa Marehemu aitwaye Deogratius Mathias John (32)Mkazi wa kijiji cha Mkajamila ambaye pia anashikiliwa na Jeshi la Polisi pamoja na mtu mwingine ambaye bado anatafutwa. 

SOMA HII; Watoto watuhumiwa kumuua mama yao kwa kumloga baba yao

Aidha, watuhumiwa wameeleza kuwa sababu ya kutekeleza tukio ni wivu wa kimapenzi baina ya Marehemu na muwewe ambapo inadaiwa marehemu alikuwa akimroga mumewe pamoja na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine. 

Credit:Mtwara Online Tv 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top