MWANAMKE AFUNGWA JELA BAADA YA KUIBA MBEGU ZA KIUME

0

 Mwanamke mmoja nchini Ujerumani amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kuiba mbegu za kiume za mpenzi wake.


Jaji wa mahakama ya magharibi mwa Ujerumani Astrid Salewski amesema mwanamke huyo alitoboa tundu kwenye kondomu za mwanaume huyo kwa makusudi ili apate ujauzito.


Uamuzi huo umetolewa katika mahakama ya kikanda katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Bielefeld.

Inaelezwa kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 39 alikuwa kwenye uhusiano mwanamume wa miaka 42 ambapo mwanamke huyo alimpenda sana mwanaume huyo lakini alijua kwamba mwanaume huyo hakutaka kupata naye mtoto

Mwanamke huyo alitoboa mashimo kwa siri kwenye kifurushi cha kondomu ambazo mpenzi wake alihifadhi kwenye meza yake ya kulalia kwa lengo la kupata ujauzito lakini juhusu za mwanamke huyo hazikufanikiwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top