NBS TUMBAKU INAUA WATU 14,700 KILA MWAKA

0

 OFISI ya Taifa ya Takwimu na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema watu milioni 2.6 sawa na asilimia 8.7 ya watanzania hutumia tumbaku ambapo zaidi ya watumiaji 14,700 hufariki dunia kila mwaka.

Watu 14,700 hufa kwa tumbaku kila mwaka - NBS

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema watu wengi huathirika na moshi wa sigara (second hand smoke) katika maeneo ya kazi, kwenye baa, kumbi za starehe na migahawa.

“Utafiti ulionyesha kuwa asilimia 77 ya watu huvutishwa sigara kwenye baa, asimilia 31.1 kwenye migahawa na asilimia 13.8 majumbani,” amesema Waziri Ummy.

Amesema kutokana na hali hiyo magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza (non-communicable diseases – NCDs) yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku na kuleta maradhi mbalimbali yanayosababishwa na matumizi holela ya bidhaa za tumbaku.

“Wagonjwa wanapokuwa wengi kwenye mahospitali na vituo vya afya inasababisha nchi kushindwa kuwahudumia ipasavyo na hivyo kusababisha vifo ambavyo vingeweza kuepukika,” amesema.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), utumiaji wa bidhaa za tumbaku husababisha vifo kwa karibu nusu ya watumiaji wake na zaidi ya watu takriban milioni 8 hufa kila mwaka duniani kwa sababu ya matumizi ya tumbaku
Milioni 7 ya vifo hivyo hutokana na matumizi ya moja kwa moja wakati milioni 1.2 ni kutokana na utumiaji wa bidhaa za tumbaku usio wa moja kwa moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top