Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), leo kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi yanayofanyika Kitaifa Dodoma, kwa niaba ya Wafanyakazi wote limemuomba Rais Samia atimize ahadi yake aliyoitoa mwaka jana ya kuwapandishia Wafanyakazi mishahara.
"Rais Samia mwaka jana ulisema 'Mimi ni Mama na Mama ni Mlezi' hivyo Mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ahadi uliyotoa katika siku ya Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka jana kuhusu kutupandishia mishahara Wafanyakazi wa Tanzania"
"Bila shaka hotuba yako hii ya leo Rais Samia itakata kiu yetu, Mama endelea kuupiga mwingi, Mama yetu mpenzi sema kitu leo ili roho zetu zitulie" Katibu Mkuu TUCTA, Henry Mkunda
Wakiwasilisha hotuba yao katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi mbele ya Rais Samia Suhumu, TUCTA imependekeza kiwango hicho ili kuwezesha Wafanyakazi na Wategemezi wao kuishi
Wamesema Kima cha Chini cha Misharaha kimendelea kuwa duni licha ya gharama za maisha kupanda, mathalani kwa Sekta Binafsi (Watumishi wa majumbani) ni Tsh. 40,000/- hadi Tsh. 60,000/-. Kwa wafanyakazi wa Umma kima cha chini ni Tsh. 315,000/-
TUCTA imefafanua kuwa Wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka 9 kwa Sekta Binafsi na miaka 7 kwa Sekta za Umma hali iliyosababisha kupungua hari ya kufanya kazi na kupunguza ufanisi mahali pa kazi
Rais Samia akizungumza kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi yanayofanyika Kitaifa Dodoma leo amesema Serikali imeunda Bodi za kushughulikia kima cha chini cha mshahara ambazo zitafanya tathmini ya kima cha chini kwenye Sekta za umma na binafsi ili kuboresha maslahi ya Wafanyakazi ambapo ameziagiza pia Wizara zinazohusika kuziwesha Bodi hizo kufanya kazi vizuri.
"Kuhusu viwango vya mishahara nakubaliana nanyi kwamba viwango havikidhi mahitaji ya Mfanyakazi na Familia yake, natambua jukumu la Bodi za kima cha chini cha mishahara, la kuishauri Serikali kuhusu kima cha chini cha mishahara"
"Serikali imeunda Bodi za kima cha chini cha mishahara ili kufanya tathimini ya kima cha chini cha mshahara kwenye Sekta binafsi na za Umma, naziagiza Wizara zinazohusika kuziwesha Bodi hizi kufanya kazi"
"Wale wote...waliokwishafanya kazi kwa muda mrefu lakini wakafukuzwa kwa ajili ya vyeti feki na kwamba hawakupata chochote cha kuondoka nacho, nimewaagiza Wizara na Wizara ya Fedha waangalie ni kiasi gani wafanyakazi wale walikatwa kwenye jasho la mishahara yao, kile walichochangia kwenye mifuko...waaangalie ni kiasi gani na waweze kulipwa jasho walilolitoa" Rais
NDUGU zangu, jambo letu lipo lakini si kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwa sababu mnajua hali ya uchumi wa nchi yetu na hali ya uchumi ya Dunia. Hali si nzuri sana, uchumi wetu ulishuka chini mno, tumejitahidi sana.
Na kwasababu nilisha toa ahadi mwaka jana, kwa hiyo nimeagiza jambo liwepo mahesabu yanaendelea tutajua lipo kwa kiasi gani lakini jambo lipo --- RAIS Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi, Mei Mosi jijini Dodoma