SHABIKI WA YANGA ATUHUMIWA KUMUUA SHABIKI WA SIMBA WAKITAZAMA MPIRA KIBANDA UMIZA.

0

Shabiki wa simba anaejulikana kwa jina la Agustino Mwangosi kutoka kijiji cha kingiri kata ya Ipinda wilayani Kyela, auwawa na shabiki wa yanga (Jina Kapuni)  kisa  ikiwa ni majibizano ya mchezaji wa Simba Peter Banda kupigwa mpira uliopita katikati ya miguu (TOBO).

Akizungumza na kyela fm katika kipindi cha KONA YA MICHEZO diwani wa kata ya Ipinda Eliah Mwaipetania, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akielezea kuwa marehemu alikuwa katika hali ya majibizano ya kishabiki na mtuhumiwa walipokuwa wakitazama mchezo wa Simba Vs Pamba katika Hatua ya robo fainali ya kombe la ASFC.

Katika majibizano hayo ilionyesha mtuhumiwa kutopendezwa na majibu ya marehemu, ndipo mtuhumiwa akaondoka eneo la tukio (KIBANDA UMIZA) na kuamua kumvizia marehemu wakati akirudi na kumuua kwa kumpiga na gogo sehemu mbalimbali za mwili na kupelekea umauti wake.

Diwani Mwaipetania amesema mwili wa marehemu umezikwa jumapili 15/05/2022 na hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.

 Diwani amewataka mashabiki wa mpira kuacha ushabiki wa hovyo na mpaka kupelekea kuuana.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top