SIKIA KAULI YA DKT GWAJIMA KUHUSU USHIRIKI WA TANZANIA MKUTANO G7

0

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima ametoa mrejesho wa mikutano miwili ya Kimataifa aliyoshiriki ikiwemo Mkutano wa 66 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali za Wanawake Duniani uliofanyika nchini Marekani na ule wa Mkutano wa G7 Care Work uliofanyika nchini Ujerumani.


Gwajima akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya Wanawake na Jinsia jijini Dodoma alisema Tanzania ikishiriki mikutano hiyo kwa lengo la kwenda kujifunza na kueleza Duniani nini Tanzania inafanya katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na Usawa wa Kijinsia.

"Mimi binafsi nilialikwa na nilishiriki katika mkutano huo ambapo niliambatana na mtaalamu mmoja. Mkutano huo ni muhimu sana kwa kuwa kama mnavyofahamu Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye aliahidi kuwa kinara wa utekelezaji wa eneo la Pili kuhusu Haki na Usawa wa Kiuchumi kwenye Jukwaa la usawa wa Jinsia" alisema Dkt. Gwajima

Aidha Dkt. Gwajima amesema lengo la Mikutano hiyo muhimu ni kujadli masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake ikiwa ni pamoja na mafanikio na changamoto zilizopo zipate maamuzi ya kisera na kiutekelezaji kutoka kwa viongozi na wataalam.

"Nimeitisha kikao hiki ili nitoe mrejesho wa mikutano hiyo miwili na pia kuweka mikakati ya utekelezaji wa maazimio ya mikutano hiyo na kupitia kikao hiki pia nitaomba tujipange vizuri zaidi ili kuwa na ushiriki bora zaidi katika mikutano hii kwa wakati mwingine" alisisitiza Dkt. Gwajima

Gwajima amewashukuru wadau waliowezesha ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 66 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali za Wanawake Duniani na ule wa Mkutano wa G7 Care Work ambao ni UN Women, UNFPA, Ubalozi wa Ireland na Asasi ya LSF, LANDESA na OXFAM ambazo zilichangia katika kuwezesha Viongozi na wataalam kushiriki mikutano hiyo.

"Ninaomba nitoe rai kwa wadau wengine wa Maendeleo kuendeleza ushirikiano huu na kutuwezesha kwa utaalam na rasilimali fedha na kushirikiana nasi katika maeneo mbalimbali kadri tutakavyoendelea kuwasiliana nao na kuwashirikisha kwenye maeneo yetu ya vipaumbele." alisema Dkt. Gwajima 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top