Simba watoa kauli kuondoka Morrison

0
Klabu ya Simba imewataka wanachama na mashabiki wao kupuuza taarifa na tetesi za mitandaoni kuwa mchezaji wao, Bernard Morrison ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

 

                                                        Kwa wiki nzima sasa kumekuwa na tetesi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hasa ya michezo, ikidai kuwa mchezaji huyo aliyesajiliwa na timu hiyo kutoka Yanga miaka miwili iliyopita, huenda akarejea huko.

Pia tetesi hizo hizo zinadai kuwa huenda klabu ya Simba ikaamua kuachana naye.

Lakini Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, ameweka wazi kuwa hakuna yeyote anayejua mpaka sasa nani atabaki na nani ataondoka kwenye klabu hiyo, mpaka hapo Kocha Mkuu, Pablo Franco atakapotoa ripoti yake baada ya msimu kumalizika, itakayoainisha nani anataka aendelee kuwa naye na yupi hamhitaji.


"Hizo tetesi za Morrison au Onyango kuhusu kuondoka zinabaki kuwa tetesi, kwetu sisi nani anaondoka, nani atabaki, ukifika muda sahihi kila kitu kitawekwa wazi na atakayebaki na kuondoka itakuwa ni kwa matakwa ya Kocha Mkuu, Pablo Franco.

"Wapo wachezaji ambao wanamaliza mikataba yao ndani ya Simba, kubali au kuondoka kunategemea na ripoti ya mwalimu, akisema nani anamtaka tutambakisha, akisema mchezaji fulani simhitaji, hata kama ana mkataba tutauvunja na kumpa mkono wa kwa kheri, Simba tumeshawahi kufanya hivyo.


"Atakayeondoka ataondoka kwa matakwa ya mwalimu kwa sababu ya kuona kuwa hatomsaidia na atakayebaki, atabaki kwa sababu ataona anafaa, hakuna anayejua nani atasalia nani atabaki, tunamwachia kocha, na hizo zote ni tetesi," alisema Ahmed.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top