TANZANIA, UNAIDS ZAKUBALIANA VITA DHIDI YA UKIMWI

0

 TANZANIA na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na masuala ya Ukimwi (UNAIDS) zimekubaliana kuendeleza ushirikiano kukabiliana na ugonjwa wa Ukimwi na maambukizi mapya.

Tanzania, UNAIDS zakubaliana vita dhidi ya Ukimwi

Hayo yamebainishwa katika kikao pembezoni cha 75 cha Shirika la Afya Duniani kati ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania mjini Geneva, Ummy alieleza kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano imara, wa kimkakati na wenye manufaa kutoka UNAIDS katika nyanja za uongozi, uundaji wa sera na ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya mwitikio wa kitaifa wa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Naye Byanyima ameupongeza uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kuwa tayari kuunga mkono azimio la kisiasa lililotangazwa na kutimiza malengo yaliyokubaliwa kwa miaka mitano ijayo katika kupambana ya Ukimwi.

Aidha, Byanyima alimshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa kinara wa  uhamasishaji wa uchangiaji wa mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).

Ummy, alielezea vipaumbele vya Tanzania katika mapambano dhidi ya Ukimwi ni pamoja na kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kuzuia maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa vijana na vijana balehe hususani vijana wa kike.

Byanyima ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kuhamasisha wafadhili wa kimataifa kutafuta rasilimali ambazo zitaleta matokeo makubwa katika kukabiliana na Ukimwi.

WANACHI WAMKATAA MTENDAJI WAO WATAKA SERIKALI IMUONDOE



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top