TCRA YASEMA GHARAMA ZA BANDO ZIKO SAWA

0

 Licha ya vilio vya gharama za vifurushi kushika kasi mitaani kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imesema gharama hizo ziko sawa na vifurushi vimepangwa vile inavyopaswa.

Mamlaka hiyo imekwenda mbele na kueleza kuwa bei ya vifurushi vya data nchini Tanzania ni ya chini kuliko nchi zote za Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Africa (SADC).

Mkurugenzi wa TCRA Dk Jabir Bakari amesema kosa pekee linalofanywa na watoa huduma ni kutotoa taarifa za mabadiliko ya vifurushi yanayofanyika kama ambavyo wanaelekezwa.

Dk Bakari amesema watoa huduma wanapaswa kutoa taarifa za mabadiliko ya vifurushi kwa wateja wake kupitia vyombo vya habari, tovuti ili isizue taharuki kwa watumiajia pindi yanapotokea mabadiliko.

SOMA HII:Samia aeleza mkakati kupunguza makali ongezeko bei ya mafuta

Kuhusu Tanzania kuwa na gharama nafuu za data amesema, "Nchi 10 zenye gharama nafuu zaidi za data ni Sudan, Algeria, Somaloa, Ghana, Libya, Tanzania, Mauritius, Nigeria, Cameroon, Senegeal. Stadi ya TCRA inaonesha gharama halisi ya kuuza data hapa nchini ni kati ya Sh2.03/Mb hadi Sh9.35/ Mb, Sh2.03/Mb ni bei ambayo Mtoa huduma anaweza kuuza data akarudisha gharama zake za uendeshaji"

"Bei ya data kwa sasa inaanzia Sh15/ MB hadi Tsh. 9.35/ MB, Tsh. 9.35/ Mb, ni bei ambayo mtoa huduma anaweza kuuza data na kutoa huduma zenye ubora na kuwafikia Wananchi wengi zaidi"amesema

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top