Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 09.05.2022

0

Halaand

CHANZO CHA PICHA,

GETTY IMAGES

Manchester City wiki ijayo ihuenda ikatangaza usajili wake ghali wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Mnorway Erling Braut Haaland, 2 (Sun)

Liverpool inaongoza mbio zinazozijumuisha pia klabu za Real Madrid na Chelsea katika kuwania saini ya kiungo mfaransa n wa Monaco Aurelien Tchouameni, 22. (Marca via Metro)

Arsenal inaweza kugonga mwamba katika mpango wake wa kumsajili mshambuliaji Muargentina Lautaro Martinez, 24 ambapo Inter Milan inaonekana haitamuuza. (Gazetta Dello Sport)

Christopher Nkunku,

CHANZO CHA PICHA,

GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Christopher Nkunku

Arsenal, Chelsea na Manchester United zinamuwania kiungo wa RB Leipzig mfaransa Christopher Nkunku, 24, msimu huu. (Football.London)

Bayern Munich inaandaa ofa ya kwanza ya £15m ili kuanza mazungumzo na RB Leipzig kwa ajili ya kiungo wake muaustria Konrad Laimer. (Fabrizio Romano on Twitter)

Hata hivyo, Manchester United pia inamtaka nyota huyo mwenye miaka 25 ambaye awali aliwahi kufundishwa na mkufunzi wa sasa wa muda wa United Ralf Rangnick. (Mirror)

Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,

GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ronaldo

Kiungo wa zamani wa Manchester United David Beckham ana matumaini mshambuliaji mreno Cristiano Ronaldo, 37, atasalia Old Trafford msimu ujao. (Talksport)

Kiungo wa zamani wa Uholanzi Fred Rutten amefichua kwamba amekataa ofa ya kuwa mmoja wa wasaidizi wa Erik ten Hag, Manchester United akijiandaa kurudi PSV Eindhoven. (Guardian)

Tottenham Hotspur itakabiliana na upinzani kutoka klabu za Bundesliga na Serie A kwa ajili ya kiungo wa Hellas Verona kutoka Czech Antonin Barak, 27. (Inside Futbal)

Liverpool wanamatumaini ya kuipiku Leeds katika usajili wa £4m wa mlinzi wa Aberdeen na Scotland Calvin Ramsay,19. Kinda huyo anaandaliwa kumsaidia Trent Alexander-Arnold. (Goal)

Meneja wa zamani wa Chelsea na Spurs Andre Villas-Boas anaweza kuwa kocha wa Morocco, na kufungua milango ya kurejea kwa Hakim Ziyech kwenye timu ya taifa. (Le360 via Sun)

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top