TUMIA NJIA HIZI 7 KUPATA FAIDA KUPITIA MTANDAO WA INSTAGRAM.

0

 Ulimwengu wa sasa unahamia kidigitali ambapo ukifanya utafiti hata ambao hauhitaji garama utagundua siku hizi hata watu wa habari kupitia redio,television au magazeti yanakutana na changamoto za kusikilizwa kutazwa au kusomwa sababu bila kuweka maudhui zaidi ya yale mtu ambayo ameyata mtandaoni basi kituo chako cha habari kitakosa wateja.

Mfano mdogo siku hizi kuna kuweka matangazo Instagram na kuyapa ufadhili yawafikie wengi au fecebook au Whatsapp,je unadhani mtu atachagua wapi kutafuta wateja wake!,nisikuchoshe twende kwenye mambo yaho nane muhimu leo.


1=TENGENEZA UTAMBULISHO (BRAND)

Tengeneza utambulisho wako au nembo (LOGO) yako inayotambulisha ofisi yako,huduma yako au bidhaa zako,hakikisha unatafuta jina zuri la kuvutia wateja wako au watembeleaji wako,weka maelezo mafupi yenye  kuvutia timilifu kwa mtembeleaji kuelewa unafanya nini,kumbuka mko wengi kwenye soko jitofautishe na wengine.


2=IFANYE KURASA YAKO KUWA YA KISASA.

Tunaposema kisasa siku hizi kizazi kinaenda kisasa sio unachukua picha nakupost na kuweka maelezo chini,wengi wao sio wapenzi wa kusoma maelezo wanatamani kupata kusoma ndani ya picha, kifupi tengeneza poster zenye mvuto,weka DP itakayokutambulisha vizuri,kumbuka kuifanya page yako kuwa ya kibiashara  BUSINESS ACCOUNT,usiweke account yako private huwezi kupata wateja na watembeleaji wengi sababu unawawekea masharti kukufikia.

3=IFAHAMU HUDUMA au BIDHAA UNATAOUZA VIZURI

linapokuja suala lingine muhimu ni kumsikiliza mteja na kumuelewesha kuhusu maswali yake,unapoifahamu vizuri bidhaa yako au huduma yako hupati shida kumpamaelezo,Jifunze kutengeneza Kicha cha bidhaa yako chakuvutia na kueleweka usisahau kuwa mwaminifu kwa wateja wako.

4=LENGA KUNDI MAALUM

Hapo ndio muhimu sana mfano wewe unadili na wanawake jitahidi sana kuwafuata (following) walengwa uwatakao,tumia hashtag sahihi ukipost mfano #ususilive #wanawakebomba #ongeanamama pia jitahidi kushiriki katika mazungumzo na wateja wako katika post kwa mtu akicoment reply aki like onesha ushirikiano kwa washirika wako.

5=KUWA MBUNIFU.

Ubunifu ni namna ya kupost maudhui yako mfano weka poster zako katika mabango,tengeneza poster kwa kufanyia Mockup katika vikombe,t-shirt n.k hakikisha poster zako ziwe safi zivutie na upekee,posterza ushauri elimu na burudani,weka stori uliza wafuasi wakokuhusu huduma zako pia huduma za bure kama ushauri hukuweka karibu na wafuasi wako.

6=JENGA JAMII YAKO.

Suala la uaminifu ndio muhimu na hakikisha uaminifu na kujali muda wa mteja wako,mzawadie msikilize na mjalimteja wako,kwa kila anayeipenda bidhaa yako jitahidi kuwa karibu nae kuchati nae kupata mawazo na maoni yake usiyapinge yapokee kisha tumia lugha za kuvutia.

7=TUMIA NJIA ZA KISASA KUFANYA BIASHARA YAKO.

Mfano katika maisha ya sasa kama nilivyotangulia kusema kuwa sasa unaweza kuyapa ufadhili matangazo yako au huduma yako kwa sponsor ads Instagram,facebook au kupitia website mbalimbali kupata wateja ambao bado hawajawa marafiki zako.

Kuna Mengi yakujifunza lakini ni bora kidogo cha kukuweka katika kesho nzuri kuliko nikakujaza elimu ukapata kusahau wapi tumeanzia jianda somo lijalo litahusu nini? mfano kuna namna ya kutengeneza pesa kupitia simu yako ukiwa nyumbani? au ungetamani kutazama video na ulipwe? endelea kufuatilia mtandao huu usisahau kutuachia maoni hapo chini.

Imeletwa kwako na Adimin.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top