Changamoto ya malezi duni pamoja na kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya wazazi na walezi kumetajwa kuwa sababu ya ongezeko la watoto na vijana wanaokuwa na tabia hatarishi zinazoweza kuendelea kuleta athari hasi katika jamii.
Miongoni mwa changamoto zilizotajwa katika mkutano wa wananchi katika kijiji cha Ulembwe wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe ni wazee kususiwa wajukuu wanaoshindwa kutekelezwa, jamii kushindwa kuwakemea watoto wanapokosea pamoja na watu wazima kujihusisha na mapenzi na vijana wadogo.
Katika mkutano na wananchi wa kijiji cha Ulembwe uliyohusisha askari wa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia ,jeshi limelenga kutoa elimu kuhusu masuala ukatili wa kijinsia pamoja na malezi katika jamii kama ambavyo Grace Nyamle ambaye ni afisa wa kitengo cha dawati lajinsia anavyoeleza.
Ili kutia mkazo na kuwafanya wananchi kubadili tabia , maofisa wa polisi akiwemo Wilfred Willa ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Njombe pamoja na Raphael Kiwuyo ambaye ni mkaguzi wa polisi wakasisitiza jamii kuachana na imani za kishirikiana ambazo zinatajwa kuhusishwa na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na akina na kisha kufanya malezi bora kwa watoto.
Kwa upande wao wananchi akiwemo Justin Kilumile wanasema Suala la mmomonyoko wa maadili kwa kiashi kikubwa linasababishwa na watu wazima ambao wamekuwa wakiwakingia kifua watoto wao wanapofanya makosa huku shida nyingine ikiwalenga watu wazima wanaojihusisha kimapenzi na watoto waliyochini ya chini ya miaka 18 hatua ambayo inahatarisha ustawi wa jamii
Jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia na watoto limejipanga kuifikia jamii zote za Njombe kwa lengo la kutokomeza changamoto ya matukio ya kikatili.
TAZAMA VIDEO HII KUHUSU KAULI YA POLISI