Faison Alimajani Sanga (19) mkazi wa kijiji cha Makwaranga kata ya Ipelele wilayani Makete anashtakiwa na Mahakama ya Wilaya ya Makete kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa shule ya msingi jina limehifadhiwa (15).
Kosa hilo la ubakaji ni kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) e na 131 (1) ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2019.
Mashaidi wawili upande wa mashtaka akiwemo muhanga mwenyewe amesema kuwa mnamo tarehe 12 Februari, 2022 mshtakiwa alimpeleka nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho huku akimuahidi ya kuwa atamuoa.
Kwa upande wa shaidi wa pili ambaye ni baba wa mtoto huyo amesema kuwa alipogundua binti yake ni mjamzito nakuamua kumpeleka kwenye kituo cha afya kwa ajili ya vipimo na ndipo alipo gundulika ni mjazito
Mshtakiwa aliposomewa shtaka lake amekana kutenda kosa hilo.
Wakati huo huo Bahati Langson Sanga mkazi wa kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama Wilayani Makete anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto ambaye jina limehifadhiwa.
Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 17 Aprili 2022 katika kijiji cha Ihanga mshtakiwa alitenda kosa hilo la kumlawiti mtoto huyo kinyume na kifungu cha 154 (1)a ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2019.
Hata hivyo amesomewa shtaka lake na kukanusha kutenda kosa hilo.
Mashauri hayo yaliongozwa na Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Makete Mh. Ivan Msaki pamoja na mwendesha mashtaka ambaye Inspecta wa jeshi la Polisi Benstard Mwoshe.
Mashauri hayo mawili yameahirishwa mpaka tarehe 30.5.2022 kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Credit:KITULO fm.