Serikali mkoani Mwanza imetoa wiki moja kwa vikundi vyote vilivyochukua mikopo kufika ofisi ya TAKUKURU kufanyiwa uhakiki wa uhai wake
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amesema kuwa vikundi vyote vilivyopokea fedha hizo za mikopo vinatakiwa kufika ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Misungwi kuhakikiwa na baada ya hapo ofisi ya mkoa ili kubaini vikundi hewa na kupata njia nzuri ya kuvisaka rasmi.
"Tumelizungumzia sana hili, sasa nawaagiza mkavipatie taarifa kwa njia yoyote hata kwa kuwapigia simu wahusika wa vikundi vyote mlivyovikopesha kufika haraka iwezekanavyo ndani ya wiki moja ili tupate kujua vikundi vipi ni hai na changamoto zao ni zipi.
Pia vikundi ambayo havitafika katika ofisi za TAKUKURU hivyo ndivyo tutaanza kupambana navyo maana ndivyo vikundi hewa vinavyotusumbua." amesema Mhandisi Gabriel.