Wabunge wacharuka ukomo matumizi ya vifurushi bando

0

Baadhi ya wabunge jana walitoa kilio chao kuhusiana na suala zima la kumalizika haraka kwa matumizi ya kifurishi cha intaneti (bando), huku wakiishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuondoa mfumo wa kifurishi cha intaneti kuisha kama zilivyo nchi nyingine.




Pia wameiomba serikali katika kipindi hiki cha kuendelea Tanzania ya kidijitali, kuhakikisha mawasiliano yanapatikana nchi nzima ikiwamo maeneo ya pembezoni.

SOMA HII;Yafahamu magonjwa ambayo ukiyapata yanakuwa ya kudumu

Waliyasema hayo jana bungeni jijini Dodoma wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba alisema Mei 13, mwaka jana, aliuliza swali lililohusu vifurushi vya mtandao ambavyo havijatumika, Waziri alisema alielekeza kampuni za simu endapo mtu kama bando lake limekwisha muda wake na akinunua lingine ule muda uliopita harudishiwi.

"Hii ninahesabu kama ni hujuma kwa Watanzania kama ndiyo wanavyofanya basi Mheshimiwa Waziri (Nape) haujatenda haki," alisema Makamba.

Akiendelea kuchangia Salome alisema Watanzania asilimia 95 wanapata mtandao na wanaweza kujiunga kupiga simu, kwamba asilimia 68 wanauwezo wa kujiunga kwenye vifurushi vya mtandao.

Alisema mtumiaji wa simu akijiunga kifurushi cha intaneti cha siku moja anapaswa atumie ndani ya muda husika, kwamba endapo akishindwa kutumia kifurushi alichojiunga ndani ya muda huo kutokana na matatizo ya mtandao hawezi kurudishiwa gharama zake alizotumia.

Alisema kampuni za simu zikifanikiwa kupata Sh. 200 tu Kwa Watanzania milioni 50 kwa siku wanaweza kukusanya Sh. bilioni 10 na kwa mwezi zaidi ya Sh. bilioni 300.

SOMA HII;Yafahamu magonjwa ambayo ukiyapata yanakuwa ya kudumu

"Mheshimiwa Waziri ameomba fedha kwa ajili ya wizara yake Sh. bilioni 282, kwa fedha hii yanaweza (kampuni) zinaweza kukusanya ndani ya mwezi mmoja tu. Sasa kusema hiyo ni biashara ni nguvu ya mazungumzo na kazi ya wizara ni kuwalinda Watanzania.

"Biashara ya kifurushi cha intaneti kuisha duniani imepitwa na wakati, nchi zilizoendelea hakuna bando kuisha muda. Kwa nini turuhusu kampuni za simu ziibe fedha za Watanzania?."

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top