MAWAZIRI WATAKIWA KUZIMA MAGARI YAO WANAPOSHUKA ILI KUBANA MATUMIZI

0

Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson, amewashauri viongozi wote nchini isipokuwa wale ambao itifaki hairuhusu, kuzima magari yao baada ya kushuka kwa sababu matumizi ya pesa kwenye eneo la mafuta yanakuwa makubwa sana kutokana na magari yao kuendelea kuwaka wakati viongozi wakiwa wameshuka. 

Spika Tulia amesema hayo  Mei 17, 2022 bungeni jijini Dodoma, amesema mfano wa Kiongozi akishuka kwenye gari na kuingia kwenye mkutano wa saa mbili lakini magari yanaendelea kuwaka kitu ambacho kinasababisha mafuta kutumika pasipo Kiongozi kuwepo kwenye gari, ameiomba Serikali kulitazama hilo na kufanya mabadiliko ili matumizi ya Serikali yapungue kwenye eneo la mafuta.

“Magari ya Viongozi ikiwa ni pamoja na Mawaziri na Manaibu Mawaziri yanaendelea kuwaka hapo nje wakati sisi tupo humu ndani, tunatamani magari ya viongozi yakishamshusha kiongozi sio tu hapa bungeni bali nchi nzima yazimwe na Dereva ashuke kwenye gari kwa sababu matumizi ya pesa kwenye eneo la mafuta yanakua makubwa sana kwa sababu ya magari kuendelea kuwaka wakati kiongozi hayupo kwenye gari ameshashuka lakini gari linaendelea kuwaka” amesema Spika huyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top