Wakazi wa Kitongoji Namba 2 Kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wameichoma moto nyumba ya mwenyekiti wa kitongoji hicho Shabani Zoro, na kuvunja nyumba ya Kamanda wa Sugusungu Buyaga Kazimoto na kuharibu mali zao zingine ikiwamo Ofisi baada ya kushikwa na hasira kusababisha mauaji ya mwenzao Jackson Joseph aliyeuawa kwa kupigwa Risasi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga ASP George Kyando, amethibitisha hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari
ASP Kyando amesema matukio hayo yametokea baada wananchi kuutuhumu uongozi huo kukithiri kuonea wananchi na kusababisha kifo cha mwenzao.
Amebainisha kuwa Mei 17 mwaka huu majira ya saa 5 usiku, marehemu Jackson Joseph (35) alikuwa na ugomvi na mkewake Ester Emmanuel (23) na baada ya ugomvi kuwa mkubwa Mwanamke alikimbilia kwa jirani kuomba msaada ndipo majirani wakapiga simu kwa Kamanda wa Sungusungu Buyaga Kazimoto, ambaye naye alichukua walinzi wanne wakampuni ya ulinzi wakiwa na silaha za moto kwenda kumkamata mwanaume huyo ndipo yakatokea mauaji.
Walinzi hao kutoka Kampuni Binafsi ya ulinzi Light Ndovu Security, walipofika nyumbani kwa Jackson Joseph alianza kuwakimbia, ndipo mmoja wa walinzi hao alimkimbiza na alipomkamata walianza purukushani akapigwa Risasi ya tumboni na kufariki dunia papo hapo.
Aidha, anafafanua kuwa baada ya tukio hilo la mauaji, kesho yake Mei 18 ndipo Wananchi wa eneo hilo wakashikwa na hasira, wakidai wamechoka kuonewa na viongozi akiwamo Mwenyekiti wa Kitongoji na Kamanda wa Sungusungu, na kuamua kuharibu mali zao ikiwamo kuchoma moto nyumba, pikipiki na kuvunja duka na Ofisi ya kitogonji.
“Jeshi la Polisi tumashikilia mlinzi wa Kampuni ya ulinzi binafsi ya Light Ndovu Securty Abdul Chacha kwa tukio hili la mauaji ya Jacskon Joseph, na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”alisema Kyando