Wananchi waliangukia jeshi la Polisi kudhibiti vitendo vya wizi mkoani Njombe.

0

 NJOMBE Wananchi wa Mtaa wa Idundilanga Mjini Njombe Wameendelea Kulalama Juu ya Vitendo vya Wizi na Udokozi unaoendelea Kukwamisha Jitihaza za kujitafutia kipato na kukuza uchumi wa familia na Taifa Kwa Ujumla. 

Wakizungumza mara baada ya Kutolewa kwa Elimu ya Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii kupitia Mkutano wa Mtaa Huo Uliolenga Kujadili zoezi la Anwani za Makazi namna ya kwenda kuweka vibao vya barabara za mitaa na Nyumba Wakazi hao akiwemo Bi.Days Milanzi na Nicholaus Chaula Wamesema Vibaka hao wamekuwa wakiwaibia mara kwa mara kwa kuvunja nyumba hata mchana na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

 Martha Mgaya ni Afisa Mtendaji wa Mtaa huo ambaye anakiri kuwapo kwa Wezi katika mtaa wake licha ya ulinzi na usalama kuanza kuimarika huku akisema wapo vijana ambao wamekuwa wakifanya doria nyakati za usiku kukabiliana na Vibaka Hao. 

Wakazi wengine wa Mtaa Huo Akiwemo Asante Mgeni na Efatha Mlowe Wanalitupia Lawama Jeshi la Polisi Kwa Kushindwa Kutoa Ushirikiano wa Kutosha Pindi Wanapopatwa na Madhira ya Wizi Katika Nyumba zao.

 Polisi Jamii Kata ya Njombe Mji Anayehudumu Mtaa wa Idundilanga Afande Mery Kweka Anatolea Ufafanuzi wa Malalamiko ya Wakazi hao ikiwemo changamoto ya kuchelewa kufika eneo la tukio na kwamba upungufu wa vyombo vya usafiri imekuwa kikwazo kwa jeshi la polisi katika kuwahudumia wananchi. 

Tatizo la Wizi Katika Mitaa Mbalimbali Mkoani Njombe Limekuwa Likitokea Mara kwa Mara na Kuzua Malalamiko Mengi Kwa Wananchi wanaolazimika Kujichukulia Sheria Mkononi Pindi Wanapowabaini Wahalifu Wao.

Na Gabriel Kilamlya 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top