WANAUME WAWILI NA MWANAMKE WAKUTWA WAMEFARIKI KIMAAJABU KITANDANI GESTI

0

 

Watu watatu waliokodi chumba cha kulala katika lodge mtaani Pipeline katika Kaunti ya Nairobi nchini Kenya wamepatikana wakiwa wamefariki dunia.


Watatu hao, wanaume wawili na mwanamke mmoja, walikodi chumba hicho mwendo wa saa sita na dakika 35 usiku wa kumkia Jumatatu Mei 9,2022 katika nyumba ya kulala wageni  ya Chairman mtaani Pipeline na kusalia chumbani humo hadi saa nane mchana. 

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mhudumu wa vyumba hivyo alienda kubaini watatu hao hawakuwa wameondoka na  mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.


 “Alienda kuwaamsha lakini baada ya kugonga kwa mlango wao hukukuwa na jibu lolote jambao ambalo lilimfanya kuarifu bosi wake na moja kwa moja kupiga ripoti kwa polisi,” taarifa ya polisi inasema.

Miili yapatikana kitandani

Polisi walipofika waliingia chumbani kwa nguvu kwa kuvunja vioo vya mlango na kuikuta miili ya wanaume wawili na mwanammke mmoja ikiwa imelala kitandani. 

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, watatu hao walikuwa wameshikana mabegani na kila mmoja alikuwa amefunga mdomo wake kwa nguvu.
 
“Hakukuwa na majeraha yoyote yanaoonekana au ishara ya vurugu. Lakini mwanamme ambaye alikodi chumba hicho kwa jina Boniface Muchiri Waruiru alikuwa ametokwa damu mdomoni na puani,” taarifa hiyo iliongeza. 

Vitambulisho viwili vya kitaifa vilipatikana chumbani humo vikiwa na majina Philip Murefu Simiyu (kuzaliwa 1959) and Boniface Muchiri Waruiru (kuzaliwa 1994). 

Miili ya watatu hao ilipelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya City inakosubiri kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha vifo hivyo.

Via Tuko News
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top