WANAWAKE 17,500 WAPATIWA MATIBABU YA FISTULA

0

 MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Macho ya CCBRT, Brenda Msangi amesema jumla ya wanawake  17,500 wamepata matibabu ya fistula tangu kuanzishwa huduma hiyo mwaka 2003.

Wanawake 17,500 watibiwa fistula CCBRT

Akizungumza leo Ijumaa Mei 20, 2022 kuelekea maadhimisho ya siku ya fistula Duniani Mei 23, Msangi amesema kwa mwaka jana wamehudumia wanawake wapatao 462.

Amesema namba hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa tatizo .

“Tukishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo serikali yetu tumefanya uwekezaji mkubwa  kwa kujenga kitengo kipya cha afya ya mama na motto, ambacho kinalenga kuwahudumia akinamama wenye historia ya fistula, wenye ulemavu pamoja na mabinti waliopata mimba za utotoni,” amesema.

Ameiomba serikali kuwepo kwa dawati lenye nembo ya CCBRT katika Stendi ya Magufuli, ili kuelekezwa hapo na kumsubiri dereva wa hospitali kuwachukua kutokana na wagonjwa hao kufika usiku na kukosa mawasiliano.

Msangi ametoa wito kwa Watanzania kila mmoja kutoa mchango kwa ajili ya kutokomeza fistula.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top