WASIOJULIKANA WACHOMA GARI LA HAKIMU.

0

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama katika Wilaya hiyo kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote wanaodaiwa kuchoma moto gari la Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda wilayani humo, Emmanuel Sheiza nyumbani kwake.

Nguvila alitoa agizo hilo Mei 9, 2022 alipotembelea eneo la tukio na baadaye kuongea na wanakijiji wa kitongoji cha Nyamilanda na kuelezea masikitiko yake.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo watu wasiofahamika walichoma moto gari la Hakimu huyo ambaye anaishi kwenye nyumba za Mahakama zilizopo jirani na Mahakama ya Mwanzo Nyamilanda.

Mkuu wa Wilaya huyo amesema "Tayari tukio hili la kusikitisha limesharipotiwa katika vyombo vya ulinzi na usalama na uchunguzi unaendelea ili kuwakamata wahusika wote na hakuna hata mmoja atakayekwepa mkono wa chuma wa sheria"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top