WAZIRI BASHUNGWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA MASASI

0

Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Apoo Tindwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kusaidia maendeleo kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.

Apoo ambaye kabla ya kuhamishiwa mkoani Mtwara alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime vijijini ambapo pamoja na watu wengine wanatuhumiwa  kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh5.6 bilioni zilizotolewa na mgodi huo kwaajili ya miradi ya maendeleo katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime.

SOMA HII:Sababu za Ole Sabaya kuachiwa huru zatajwa na Mahakama

Bashungwa amtengaza maamuzi hayo leo Mei 6, 2022 katika kijiji cha Genkuru wilayani Tarime baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Genkuru kilicho gharimu zaidi ya Sh700 milioni ambacho hadi sasa hakijakamilika licha ya kugharimu kiasi hicho cha fedha, fedha ambazo ni sehemu ya fedha za CSR.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top