Wananchi wa Kijiji cha Yakobi kilichopo katika kata ya Yakobi Wilayani Njombe mkoani Njombe wamemtaka mwananchi mwenzao aliyefahamika kwa jina la Mzee Gerhad Makinda kuhama kijijini hapo kwa kile wanachodai kuwa amekuwa akipora mashamba ya watu na kuwanyanyasa wananchi.
Akisoma taarifa ya kijiji Mtendaji wa kijiji hicho Alex Chriford amesema mwananchi huyo amekuwa si muungwana katika kuishi na wenzake kijijini hapo kwani amekidanya matukio yasiyo mazuri ikiwemo kupora mashamba, kulisha mifugo kwenye madhamba ya wenzake pamoja na mbwa wake kung'ata mifugo ya wenzake.
Baada ya kusikiliza mvutano huo mkuu wa Wilayani ya Njombe Kissa Kasongwa anatoa agizo la kuteua basdhi ya wazee maarufu ili wakae na kuzungumza na mzee huyo lakini kila aliyeteuliwa alikataa kwa madai kuwa mzee huyo si muelewa.
TAZAMA VIDEO HII WANANCHI WAKIMFUKUZA MWENZAO MBELE YA DC