AFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA KUMBAKA MWANAYE

0

Mahakama ya wilaya ya Iringa imemhukumu kifungo cha miaka 30 na fidia ya shilingi milioni moja Kumbuka Mhotelwa mwenye umri wa miaka 30 mkulima na mkazi wa Kitwiru wilaya ya Iringa kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi Emmy Msangalufu amesema mtuhumiwa amekutwa na Hatia ya  kutenda kosa hilo tarehe 19/11/2020 ambapo mtuhumiwa alikuwa akiishi na mke wake ambaye alikuwa mgonjwa na alikuwa na kawaida ya kushtuka usiku ili kuweza kunywa maji.

Taarifa ya Mke wake imeeleza kuwa siku ya tukio alishtuka usiku na kukuta mumewe hayupo kitandani na alipotazama sebuleni akamuona mumewe akiwa anambaka mwanaye aliyekuwa na umri wa miaka 6 huku pembeni yake kukiwa na mtoto mwingine mwenye umri wa miaka mitatu na alikuwa macho akishuhudia baba yake akimbaka dada yake.

Baada ya kushuhudia hivyo alipiga kelele kumkataza mumewe asiendelee na tukio hilo lakini haikusaidia kwa sababu mke alikuwa hawezi kusimama na hivyo kushindwa kumzuia kuendelea kubaka.

Baada ya kumaliza Tukio hilo Mtuhumiwa alimtisha mke wake kuwa endapo atasema popote basi atamuua.

Hata hivyo baada ya kupambazuka mkewe alikwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi ndipo mtuhumiwa akakamatwa na mtoto akapelekwa hospitalini ndipo walipothibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa amebakwa kutokana na kuwa na michubuko.

Kesi hiyo imeendeshwa na wakili wa serikali Allice Thomas na Jackline Nungu, Katika utetezi wake mtuhumiwa aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu hiyo kwa sababu alikuwa haelewani na ndugu wa mke wake hivyo kuamini ndio  wamemtengenezea kesi hiyo.

Licha ya maombi hayo mahakama ikampa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela pamoja na fidia ya shilingi million1.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top