AJALI NYINGINE MWANAFUNZI AGONGWA NA GARI LA SHULE AFARIKI

0

 

Gari lililopata ajali na kuua mtoto wa shule mwenye umri wa miaka 4

JESHI la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia dereva wa gari la Shule ya Msingi Samuu, Kassim Said Mahona (40) kwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo Godlight Chisawilo (04) kwa kumgonga na gari la shule hiyo Mjini Shinyanga.

 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatano Juni 22,2022 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando  tukio hilo limetokea jana Jumanne Juni 21,2022 majira ya saa 12 jioni katika maeneo ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga.

 

“Gari lenye namba za usajili T.151 DAG Toyota Coastar mali ya Malatia wa Shinyanga likitokea shule ya msingi Samuu kuelekea Majengo Mapya likiendeshwa na dereva aitwaye Kassim Said Mahona (40) na mkazi wa Nguzo Nane Shinyanga, lilimgonga mtembea kwa miguu Godlight Chisawilo (04) mwanafunzi wa shule ya chekechea Samuu na kumsababisha kifo chake,” ameeleza Kamanda Kyando.

 

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara na tayari mtuhumiwa amekamatwa.

 

Habari kutoka eneo la tukio zinasema mwanafunzi huyo amegongwa na gari hilo baada ya kushushwa na gari hilo akitokea shuleni.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top