AJALI NYINGINE YATOKEA SHINYANGA,BASI LATUMBUKIA MTONI

0

Watu watatu wamefariki dunia huku saba wakijeruhiwa baada ya Basi la Zuberi linalofanya safari za Mwanza - Kahama kugonga kingo za daraja na kupinduka katika eneo la Mwigumbi Mkoani Shinyanga.

 

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Juni 15, 2022 majira ya saa nane mchana katika barabara ya Mwanza Shinyanga ambapo basi hilo lenye namba za usajili T435 DJS SCANIA liligonga ukingo wa daraja la Mwigumbi na kutumbukia bondeni.


Kamanda Kyando ametaja mmoja wa waliofariki dunia kuwa ni dereva wa basi hilo aliyefahamika kwa jina la Hamza Haule.


Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva alipata tatizo la kiafya akiwa safarini.


Aidha, ametoa wito kwa madereva kuchunguza afya zao kabla ya kuanza safari ili kuepusha ajali zisizo za lazima.Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top