AJALI YA TRENI WANNE WAFARIKI DUNIA YAJERUHI WENGINE 132

0

Watu wanne wamefariki dunia katika ajali ya Treni iliyotokea leo mkoani Tabora ambapo kwa mujibu wa shirika la Reli Tanzania limesema  kuwa Treni ya abiria namba Y14 yenye injini namba 9019, iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, imepata ajali majira ya saa 5:00 asubuhi eneo la Malolo mkoani Tabora Juni, 22,2022.

Picha za ajali ya Treni leo juni 22 2022

Imeelezwa kuwa Treni iliondoka Stesheni ya Kigoma majira ya saa 2 usiku, siku ya Jumanne tarehe 21 Juni 2022, kuelekea Dar es salaam ikiwa na behewa 8 zilizobeba abiria 930. lipofika eneo la Malolo (Km 10 kutoka stesheni ya Tabora) behewa 5 za abiria daraja la tatu, behewa 1 la vifurushi, behewa 1 la huduma ya chakula na vinywaji na behewa la breki zilianguka na kusababisha ajali.


Majeruhi 132 tayari wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa, Kitete Tabora, kwaajili ya matibabu na wanaendelea vizuri. Ajali imesababisha jumla ya vifo 4 wakiwemo watoto 2, wakike mwenye umri wa miaka 5 na wakiume miezi 4 na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke.


Shirika linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam.

Shirika la Reli linaendelea kufuatilia kwa karibu, kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua.TRC inatoa pole kwa familia za marehemu na linawaombea majeruhi wa ajali wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.

TRC itaendelea kuutaarifu umma endapo kutakuwa na taarifa nyingine zitakazojitokeza katika eneo la ajali.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top