AJERUHIWA KWA KUCHELEWA KUREJESHA VIATU ALIVYOAZIMA KWA JIRANI YAKE

0

 Mwanamume mmoja aliyefahamika kwa jina la Museje Bejai mwenye umri wa miaka 35, amejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na jirani yake kufuatia mzozo ulioibuka kuhusu viatu vya kuazima katika eneo la Likoni, Mombasa.


Ripoti ya polisi inaeleza kuwa Bejai alivamiwa na jirani yake aitwaye Rua Masika baada ya mdogo wake Museje kushindwa kumrudishia viatu alivyoazima ili avae kwenda kanisani.

Imeelezwa kuwa, Mshtakiwa huyo akiwa na hasira, alivamia nyumba ya Bejai akitaka kujua kwa nini kaka yake aliyeazimwa viatu hakurudisha viatu hivyo kama walivyokubaliana.

Kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Stephen Matu akithibitisha kisa hicho alisema, Masika hakumkuta nyumbani hapo kijana aliyemwazima viatu, hivyo mzozo ukaanza baina ya kaka yake na mwazimaji wa viatu hivyo.

Makabiliano yalizuka kati ya Bejai na Masika kabla ya mtuhumiwa kumshambulia kwa kuchomoa panga lake na kumjeruhi mwathiriwa kwenye mkono wa kushoto.

"Mshukiwa alimvamia mwathiriwa kufuatia mabishano kuhusu ni kwa nini mdogo wake alishindwa kurudisha viatu alivyoazima kama walivyokubali awali," mkuu wa polisi alisema.

"Hata hivyo baada ya kufika nyumbani kwa mwathiriwa, aligundua kuwa rafiki yake alikuwa ameondoka na viatu havipo nyumbani, mabishano yalizuka na yeye (mtuhumiwa) alitoa panga na kuutumia kumkata mkono wa kushoto."

Matu alithibitisha kuwa mshukiwa huyo amekamatwa na anashughulikiwa kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu shtaka la kusababisha madhara makubwa.

Bejai alitibiwa katika hospitali ya Manyatta katika kaunti ndogo ya Likoni na baadaye kuruhusiwa kuenda nyumbani.

ISIKUPITE VIDEO HII TAFADHALI BOFYA HAPA KUTAZAMA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top