ALIYEVULIWA UMEYA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA TENA,,,ADAI MOSHI IMELALA

0

 MEYA wa zamani wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu, aliyevuliwa wadhifa huo baada ya kupigiwa kura za siri na madiwani za kukataliwa amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo.

Juma Raibu aling'olewa katika wadhifa huo Aprili 11 mwaka huu, baada ya madiwani kupiga kura za siri na kati ya kura 28 zilizopigwa, 18 zilikataa asiendelee na wadhifa huo huku 10 zikimtetea abaki katika nafasi hiyo aliyodumu nayo tangu ulipokamilika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Tuhuma zilizomng'oa Raibu ni madai ya kuhudhuria sherehe ya kijana mmoja anayedaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja, kutumia vibaya ofisi yake, kujihusisha na vitendo vya rushwa, kuruhusu ujenzi holela na kutumia fedha nje ya utaratibu.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Moshi mjini, Raibu amesema ameamua kurudi kuwania nafasi hiyo kwa kuwa toka ameondolewa kwenye nafasi hiyo, baada ya kuona Moshi imepoa na kuwepo kwa vurugu nyingi.

'Moshi imelala, siyo Moshi niliyokuwa nikiiongoza, nimeona ni wakati wa kurudi kuchukua nafasi hii, ninaamini tutashirikiana na madiwani katika kuiendeleza Moshi'

WASIOJULIKANA WAMUUA MTOTO KWA KUMCHINJA SHINGO,MAMA AKIWA MSIBANI



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top