![]() |
PICHA KUTOKA MAKTABA |
Akizungumza na kitruo cha redio @wasafifm mwenyekiti wa wa mtaa huo Michael John amekiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake nakusema kuwa baada ya kutokea kwa mauaji hayo alichukua jukumu la kuzungumza na mtuhumiwa sababu ya kuchukua jukumu la kumuuwa binamu yake nakusema alimkuta marehemu yupo na mke wake chumbani wanafanya mapenzi ndipo mtuhumiwa akachukua kisu na kumchoma upande wa kushoto wa kifua bila kukusudia
Pia tumefanikiwa kuzungumza na mama wa marehemu Agnesi Yona ambae amesema amekuja kujua kifo cha mtoto wake baada ya kuambiwa na mwenyekiti akiwa anaenda kwenye shughuli zake hivyo amelaani tukio hilo kwakuwa marehemu na mtuhumiwa ni mtu na ndugu yake
Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo lilitokea nyumbani kwa mtuhumiwa ambapo marehemu alikua na mke wa mtuhumiwa ndipo alipokutwa mara baada ya mtuhumiwa kurudi nyumbani kwenda kuchukua vifaa vya kazi yake
Licha ya mtuhumiwa kujisalimisha mwenyewe kituoni @wasafifm tunaendelea kufuatilia tukio hili kwa upande wa jeshi la polisi ili kujua kauli yao juu ya tukio hilo.
Chanzo;Wasafi fm
USIPITWE NA VIDEO ZETU KWENYE YOUTUBE YETU TAFADHALI BOFYA VIDEO HII