AMUUA MWENZAKE KWA RISASI,WIVU WA MAPENZI WATAJWA CHANZO

0

 RAIA wa china Zheng Lingyao (42), anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26), ambaye pia ni raia wa China, mfanyabishara na mkazi wa Kalenga, Ilala Dar es Salaam, huku uchunguzi wa awali ikidaiwa ni masuala ya mapenzi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema  kuwa tukio hilo lilitokea Juni 11, 2022 Mtaa wa kalenga, kwenye ghorofa ya tatu saa 5:45 usiku.

Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqin (32), raia wa China na badaye alimfyatulia risasi Fu, raia wa China ambaye alipoteza maisha. Nie anaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).amesema Muliro

“Uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi,” amesema Kamanda Muliro.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top