ANUNUA JENEZA JIPYA LA MILIONI 1.2 AKIJIANDAA NA MAZISHI YAKE

0

 


Mzee mmoja kutoka kaunti ya Busia nchini Kenya amewaacha wenyeji vinywa wazi baada ya kujinunulia jeneza la tatu.

Alloise Otieng' Ominang'ombe mwenye umri wa miaka 87 amenunua jeneza jipya la thamani ya KSh 58,000  sawa na shilingi 1,218,000 za Tanzania na ambalo anatazamia kutumia kama gari lake la mwisho duniani.

Mzee huyo anatoka katika kijiji cha Kajoro huko Okatekok, eneo bunge la Teso Kusini kaunti ya Busia.

 Alikuwa amenunua majeneza mengine mwaka 2009 na 2012; hata hivyo alisema yalikuwa yamepitwa na wakati ikilinganishwa na mtindo wa sasa wa kuunda majeneza.

Aliambia runinga ya Citizen kwamba majeneza ya awali yatapasuliwa kuwa vipande vya kuni wakati wa mazishi yake, huku lile alilonunua jipya likitumika katika kumzika.

 "Mawili hayo yatapasuliwa vipande vipande ili vitumike kupika wakati wa mazishi yangu," alisema.

“Nataka hili liwe funzo kwa jamii yangu kwa ujumla. Unaweza kukosa mahitaji ya msingi ukiwa hai. Lakini ukifa, watu watachinja ng'ombe, watakununulia nguo nzuri na viatu wakati utakuwa umeenda kabisa. Ndiyo maana niliamua kupanga jinsi safari yangu ya mwisho itakavyokuwa inayolingana na hadhi yangu katika jamii,” aliongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top