AUAWA BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA ANAYEDAIWA KUWA NI MPENZI WAKE

0

Mkazi wa kijiji cha Kiziwa kata ya kiloka wilaya ya Morogoro anayejulikana kwa jina la Kibwana Mussa amekutwa ameuawa kwa kukatwa na na vitu vyenye ncha kali nyumbani kwa mwanamke anayejulikana kwa jina la Farida Ally inayesadikika kuwa ana mahusiano naye ya kimapenzi.


Akizungumzia kuhusu tukio hilo mwanyekiti wa kijiji hicho Mbena Loki amesema tukio hilo lilitokea Juni 22 mwaka 2022 huku mwenyekiti akieleza kuwa inadaiwa Marehemu ameuawa na mme wa mwanamke aliyekutwa nae.

Mwenyekiti ameongeza kuwa mwanamke huyo kwa mda mrefu aliachana na mme wake (anaedhaniwa kutenda tukio hilo) jambo lililopelekea kuanzisha mahusiano na marehemu.

Mwenyekiti ameongeza kuwa siku ya tukio mme wa mwanamke huyo aliwavizia na kuwakuta ndani na kuamua kumshambulia marehemu hadi kupelekea kifo.

Kwa upande wa Jeshi la polisi kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu akizungumza kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top